Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, Muhammad Sayyid Tantawi, Sheikh wa al-Azhar ameafiki kuanzishwa kwa kitengo hicho kutokana na ombi la serikali ya Sudan na kusisitiza kwamba, hakuna kizuizi chochote cha kutekelezwa ombi hilo, kwa kuzingatia kuwa nchi mbili hizo za Kiislamu zina uhusiano mzuri. Tantawi ameongeza kwamba, kufikia sasa kituo hicho muhimu cha Kiislamu kimeandaa semina na warsha kadhaa za kutoa mafunzo kwa maimamu wa misikiti na wahubiri wa dini ya Kiislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia na kwamba kiko tayari kuandaa semina kama hizo za mafunzo kwa wahubiri wa Sudan.
Tantawi amesema, kitengo hicho kitakuwa na jukumu muhimu la kuimarisha ushirikiano kati ya Misri na Sudan katika nyanja za mafunzo na elimu ya kidini na kwa shabaha ya kueneza mbinu za mafunzo za al-Azhar nchini Sudan.
Huku akisisitiza kwamba Sudan ina haja kubwa ya kunufaika na msaada wa al-Azhar katika kutoa mafunzo ya kidini kwa wahubiri wa nchi hiyo, Mina Arkui Minawi, mmoja wa washauri wa Rais Omar al-Bashir ambaye amewasilisha ombi la kuanzishwa kitengo hicho kwa viongozi wa al-Azhar amesema kuwa, kuwepo ushirikiano na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wanafikra na wasomi wa Sudan na wanazuoni wa al-Azhar kuhusiana na taaluma za itikadi, fiqhi na juhudi kwa ajili ya kuenezwa fikra za Kiislamu nchini humo ni miongoni mwa malengo ya kuasisiwa kitengo hicho muhimu cha al-Azhar nchini Sudan. 367157