Chama cha mrengo wa kushoto cha Uhispania kimedai kuwa uamuzi wa Wizara ya Elimu wa kuruhusu mafunzo ya malezi ya Kiislamu katika shule za miji ya Sebta na Melilla unaonyesha jinsi serikali ilivyosalimu amri mbele ya matakwa ya jumuiya na taasisi za Kiislamu.
Chama hicho pia kimeitaka serikali kuu ya Uhispania kutupilia mbali uamuzi huo kwa madai kwamba dini inapaswa kuwa mbali na shule na vituo vya elimu.
Wiki iliyopita Wizara ya Elimu ya Uhispania iliruhusu suala la kutolewa mafunzo ya malezi ya Kiislamu katika shule za miji ya Sebta na Melilla, suala ambalo limeakisiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari vya Uhispania.
Wizara ya Elimu ya Uhispania imetangaza kuwa imeainisha kundi la waalimu wanaoijua vizuri lugha ya Kihispania kwa ajili ya kutoa elimu ya malezi ya Kiislamu katika shule na vituo vya elimu nchini humo. 367262