Mkuu wa Idara ya Maeneo Matakatifu ya Ziara katika Jumuiya ya Hija na Ziara nchini Iran amesema, kila siku idara hiyo hupokea maombi ya watu elfu 10 wanaotaka kwenda kufanya zira huko Karbala nchini Iraq.
Hussein Akbari amesema kuwa kwa kuzingatia suala hilo, idadi ya watu wanaokwenda kufanya ziara nchini Iraq itaongezeka na kufika watu elfu 4 kwa siku.
Amesema katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, takriban watu 2,700 wamekuwa wakienda ziara nchini Iraq kwa siku na kwamba idadi hiyo itafika elfu 4.
Mkuu wa Idara ya Maeneo Matakatifu ya Ziara katika Jumuiya ya Hija na Ziara nchini Iran amesema, tatizo kubwa la kupeleka watu kufanya ziara nchini Iraq ni ukosefu wa suhula za kutosha nchini humo. 367095