Kufuatia kukadhibishwa kwa habari ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, ya kumtumia barua Rais Barack Obama wa Marekani, serikali ya Washington imeiandikia barua rasmi harakati hiyo ikitaka kujua ukweli wa mambo kuhusiana na suala hilo.
Serikali hiyo inawataka viongozi wa Hamas kujibu rasmi madai yanayotolewa kuhusiana na wao kuiandikia barua serikali ya Washington.
Siku ya Alkhamisi iliyopita, wakati Seneta John Kerry wa Marekani alikuwa akiongoza ujumbe wa maseneta wa nchi hiyo katika safari yao huko Gaza, Ahmad Yusuf, Mshauri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Hamas, aliandika barua kwa jina la Hamas na kumkabidhi Kerry bila ya kuwashauri viongozi wa Hamas ili aikabidhi kwa Rais Obama, lakini serikali ya Waziri Mkuu Hania imekanusha kuandika na kutuma nchini Marekani barua kama hiyo.
Vilevile vyombo vya kuaminika kutoka ukanda huo vinasema kuwa, barua hiyo aliyotumiwa Obama ni ya mtu binafsi na wala haina uhusiano wowote na serikali ya Hamas. 367785