Akizungumzia suala hilo, Adel Dhurabb, mmoja wa maafisa wa Hamas amesema kuwa maafisa wa Misri wameruhusu idadi hiyo ya Wapalesina kuvuka mpaka na kuingia katika ardhi ya nchi hiyo, wakiwa ni wanafunzi au Wapalestina walio na hati za kuishi katika nchi hiyo au katika nchi nyingine.
Serikali ya Misri ilifunga kivuko hicho mwezi Juni mwaka 2007, lakini imekuwa ikikifungua mara kwa mara kwa lengo la kuwaruhusu Wapalestina kutekeleza shughuli zao kwa muda mfupi tu. Utawala haramu wa Israel pia umeuzingira kikamilifu Ukanda wa Gaza na baadhi ya wakati umekuwa ukiruhusu kuingizwa katika ukanda huo bidhaa za dharura tu kama vile maji na madawa. Hilo limekuwa likifanyika kutokana na mashinikizo makubwa ya kimataifa. 368250