IQNA

Kikao cha benki za Kiislamu mjini London

11:27 - February 25, 2009
Habari ID: 1748283
Kikao cha mfumo wa benki za Kiislamu kimefanyika Jumanne mjini London Uingereza. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, idadi kubwa ya watafiti, wanasheria na wawekezaji wamekutana mjini London kwa ajili ya kuchunguza mustkabali wa sekta ya mfumo wa benki za Kiislamu.
Lengo kuu la kikao hicho ni kuchunguza mazingira ya hivi sasa ya ulimwengu wa uchumi, kuchunguza udhaifu na matatizo yanayoukabili mfumo wa benki za Kiislamu na kuwasilisha njia za kukabiliana na jambo hilo.
Kikao hicho vile vile kimechunguza njia za kuwashirikisha watu wasiokuwa Waislamu katika mfumo huo, maombi ya kutolewa hawala za Kiislamu kutoka nchi zisizo za Kiislamu na hamu yao ya kuanzisha taasisi zinazotegemea mifumo ya kifedha ya Kiislamu.
Benki za Kiislamu ambazo huendesha shughuli zao kwa kutegemea sheria za Kiislamu zimeepuka mgogoro wa kiuchumi ambao umeziathiri kwa kiwango kikubwa benki zilizosimama juu ya misingi ya mifumo ya kifedha ya Magharibi. Hata hivyo, zimeathiriwa kwa kiwango fulani kutokana na kupungua kwa uwekezaji wa kigeni. 369039
captcha