Umati mkubwa wa wananchi na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) ulihudhuria maombolezo hayo ambayo yalifanyika siku ya Jumanne usiku.
Watu waliohudhuria maombolezo hayo hatimaye walishiriki katika swala za jamaa za Magharibi na Ishaa huku wakiwa na majonzi na huzuni kubwa.
Maombolezo kama hayo pia yamefanyika katika kaburi hilo siku ya Jumatano usiku kwa lengo la kukumbuka kuuawa shahidi Imam wa nane wa Madhehebu ya Shia, Imam Ali bin Musa ar-Ridhaa (as). 369438