IQNA

Spika wa Bunge la Iran awataka Waislamu kulinda umoja na mshikamano

10:43 - February 28, 2009
Habari ID: 1749251
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu Sheikh Yusuf Qardhawi akisisitiza zaidi ya udharura wa kulindwa umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Dakta Ali Larijani ameashiria hali ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu hususan katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina baada ya mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel na akasisitiza juu ya kushikamana zaidi umma wa Kiislamu.
Dakta Larijani amesema kuwa wanazuoni wa Kiislamu wana nafasi kubwa katika uwanja huo na kuongeza kuwa maulamaa wanaweza kutoa mchango mkubwa katika kuimarisha mshikamano na umoja wa Kiislamu. Spika wa Bunge la Iran amemwalika Sheikh Qardhawi kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina utakaofanyika mjini Tehran tarehe 4 na 5 mwezi ujao wa Machi. Mkutano huo umetayarishwa na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu Sheikh Yusuf Qardhawi amesema kuwa suala la Palestina ndio kadhia ya kwanza ya ulimwengu wa Kiislamu na ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa juhudi zake katika kuwaunga mkono na kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. 369729
captcha