IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya wanafunzi yaanza nchini Qatar

10:59 - March 01, 2009
Habari ID: 1749651
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kwa wanafunzi wa Qatar yameanza nchini humo leo Jumapili chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu ya Juu ya nchi hiyo. Mashindano hayo yanafanyika katika makundi mawili ya wanawake na wanaume.
Gazeti la nchi hiyo la As-Sharq limeandika kuwa wanafunzi wa kike na kiume wapatao 16,317 kutoka shule zote za serikali na zisizo za serikali watashindana katika mashindano hayo na zawadi kutolewa kwa washindi, ili kuwashajiisha wazingatie na kujifunza elimu mbalimbali za Qur'ani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati inayoandaa mashindano hayo, mashandano hayo yatagawanywa katika sehemu mbili za shule bora na za binafsi na sehemu ya pili itahusiana na wanafunzi waliohifadhi juzuu saba hadi 30 za Qur'ani. 370119
captcha