Hayo yamesemwa na Mkuu wa Siasa za Kigeni wa umoja huo Javier Solana ambaye juzi alilitembea eneo la Ukanda wa Gaza ikiwa ni mara ya kwanza tangu harakati ya Hamas ishinde uchaguzi wa Bunge la Palestina zaidi ya miaka miwili iliyopita. Solana amesema kuwa Umoja wa Ulaya uko tayari kusaidia juhudi za kulijenga upya eneo la Gaza lililoharibiwa kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel.
Solana aliwasili Gaza huku viongozi wa makundi mbalimbali ya Kipalestina wakiendelea na mazungumzo ya kutatua hitilafu zao na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Amesema Umoja wa Ulaya unasubiri matokeo ya mazungumzo hayo na kwamba utachukua hatua kwa mujibu wa matokeo hayo.
Zaidi ya Wapalestina 1300 waliuawa katika mashambulizi ya kinyama ya siku 22 yaliyofanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza. Watu wengine zaidi ya elfu tano walijeruhiwa na nyumba zaidi ya elfu nne ikiwemo zaidi ya misikiti 30, ziliharibiwa. 370157