IQNA

Kitabu cha 'Maudhui za Qur'ani' chachapishwa nchini Russia

10:36 - March 02, 2009
Habari ID: 1750213
Kitabu chenye anwani ya 'Maudhui za Qur'ani' kimechapishwa kwa lugha ya Kirusi kwa udhamini wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow.
Sakir Ahmad, mwandishi wa kitabu hicho amezungumzia kwa ufupi na kwa lugha nyepesi maana ya sura za Qur'ani Tukufu.
Mwandishi anasema katika kitabu hicho kwamba, Qur'ani ni mwongozo wa watu wote duiani wakiwemo Wakristo, Mayahudi na hata wanaopinga kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Mabudha na wasiokuwa na dini.
Kitabu hicho kimepachapishwa na Shrika la Uchapishaji la Ilya. 370842
captcha