IQNA

Ihsanoglu apongeza mazungumzo ya makundi ya Palestina

15:48 - March 03, 2009
Habari ID: 1751232
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu OIC amepongeza mazungumzo yanayofanyika kati ya makundi mbalimbali ya Palestina kwa ajili ya kuimarisha umoja na kuchunguza uwezekano wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Prf. Ekmeleddin Ihsanoglu amesifu juhudi zinazofanywa na serikali ya Misri kwa ajili ya suluhu kati ya makundi mbalimbali ya Palestina na akasema ana matumaini kwamba mazungumzo hayo yatakuwa hatua muhimu katika njia ya umoja na mshikamano wa kitaifa huko Palestina ili raia wa eneo hilo wapate kuishi katika amani na utulivu.
Katibu Mkuu wa OIC ameongeza kuwa mazungumzo kati ya makundi ya Palestina yanapaswa kuwapa Wapalestina fursa ya kupata haki zao za kibinadamu na za kimsingi na kuunda dola huru.
Ihsanoglu ameyahamasisha makundi yote ya Palestina kushiriki kwenye kikao cha Cairo na kukomesha hitilafu zao kwa lengo la kuunda serikali moja. Vilevile amewataka wananchi wa Palestina kuungana katika kuijenga upya nchi yao hususan eneo la Ukanda wa Gaza. 371578
captcha