Akizungumza katika mji mtakatifu wa Qum, Farisi amesema kuwa hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaagiza elimu ya ubinadamu kutoka nje kuliko yenyewe kuizalisha elimu hiyo humu nchini. Amesema, ili kurekebisha jambo hilo na kuifanya Iran kuwa nchi inayozalisha elimu hiyo, kuna kundi maalumu ambalo limeundwa ili kushughulikia jambo hilo.
Amesema, hadi leo bado Jamhuri ya Kiislamu inatumia vitabu vya elimu ya ubinadamu vilivyoandikwa na wanafikra wenye kiburi wa nchi za Magharibi na kwamba bila ya kusoma vitabu hivyo wasomi wengi hapa nchini hawawezi kutambua vyema maadui wao katika zama hizi.
Akizungumzia Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Jalal Deen Farisi amesema kuwa mapinduzi hayo yalifanikisha masuala mawili muhimu, la kwanza likiwa ni kuuangusha utawala dhalimu wa Shah uliokuwa ukiungwa mkono na kupewa himaya ya moja kwa moja na serikali ya Marekani na la pili ni kuleta mabadiliko makubwa katika eno zima la Mashariki ya Kati.
Amesema, katika kipindi cha kudhihiri ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Imam Khomeini ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi hayo, hakuwacha nafasi ya kuzibwa pengo la utawala nchini na fikra za Kimaksi na kikomunisti kutoka kambi ya Urusi ya zamani. Kuhusiana na suala hilo, Farisi amemtaja Imam Khomeini kuwa mtaalamu mkubwa zaidi wa Umaksi nchini lakini kwamba, licha ya hayo jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna mtu yoyote anayezungumza na kuliweka wazi jambo hilo.
Amesema kuwa Imam Khomeini alikuwa akiuchukulia Umaksi kuwa hatari kubwa hata kuliko siasa za Wamarekani. Amesema, kuhuishwa na kuimarika tena kwa fikra za Kimaksi ulimwenguni ni hatari kubwa kwa sababu viongozi wa fikra hizo wangali wana vituo muhimu vya utafiti na kisiasa katika nchi za Ulaya Mashariki na vilevile nchini Russia kwenyewe. 371943