Mashindano hayo ambayo yamepewa jina la "Zawadi ya Mfalme Muhammad wa Sita" yanafanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) na yatawashirikisha washindani kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Morocco imesema, mashindano ya awali ya Qur'ani ya Zawadi ya Mfalme Muhammad wa Sita yalifanyika tarehe 14 na 15 Oktoba mwaka 2008 mjini Rabat na waliofaulu katika mashindano hayo ndio waliopata tiketi ya kuingia mashindano ya sasa.
Mashindano hayo yalifunguliwa jana katika chuo cha Qur'ani cha msikiti wa Hassan wa Pili katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa kisiasa na kidini. 372308