IQNA

Usalama wa kiroho una athari kubwa katika usalama wa kimwili

12:56 - March 05, 2009
Habari ID: 1752032
Huku akibainisha kuwa usalama wa kimaanawi na kiroho una athari kubwa katika usalama wa kimwili, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa watu walio salama kamwe huwa hawakabiliwi na udhaifu wa kiroho wala kimwili kutokana na ukweli kwamba, imani ya kimaanawi ina nafasi kubwa katika kuimarisha azma ya mwanadamu na kufanya ayashinde magonjwa mbalimbali.
Akizungumza hivi karibuni mbele ya Mawaziri wa Afya wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC, Rais Ahmadinejad amesema kuwa bila usalama wa kimwili na kimaanawi, maisha ya mwanadamu huwa hayana ladha kabisa.
Rais Ahmadinejad amesema kuwa jambo hilo lina umuhimu mkubwa kwa jamii ya mwanadamu na kwamba usalama wa kimwili ni utangulizi wa maisha bora yenye furaha, ukamilifu na utanashati kwa mwanadamu.
Ameendelea kusema kuwa, iwapo mja ataishi maisha yaliyosimama kwenye msingi wa mafundisho ya kidini na kimaanawi, atakabiliwa na maradhi na matatizo machache mno ya kimwili. Amesema, tunapasa kuwa waangalifu wa miili yetu katika upande mmoja na katika upande wa pili kueneza mafundisho ya kimaanawi na Kiislamu duniani. 372829
captcha