IQNA

Mahdi Sotudeh: Sanaa itumike kueleza masuala ya kidini

21:04 - March 05, 2009
Habari ID: 1752141
Masuala ya kidini yanapaswa kuelezwa kwa kizazi cha vijana kwa kutumia wenzo wa sanaa kwa sababu lugha ya sanaa ndiyo yenye mvuto zaidi na yenye uwezo wa kufikisha kwenye lengo katika njia ya kulingania dini na Qur'ani kwa njia sahihi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya mkoa wa Ardebil kaskazini magharibi mwa Iran, Mahdi Sotudeh ambaye ameongeza kuwa mtazamo wa Waislamu kuhusu kitabu kitakatifu cha Qur'ani unapaswa kubadilishwa ili waweza kufaidika na mafundisho ya kito hicho chenye thamani kubwa.
Bwana Sotudeh amesema kuwa familia zinaweza kutoa mchango mkubwa katika kuwaelimisha vijana utambulisho wao wa Kiislamu, kuwaonyesha vigezo bora, mwenendo mzuri na utamaduni wa Kiislamu.
Amesema kuwa wazazi wanapaswa kutambua mahitaji ya kiroho ya watoto wao na kuwafunza utamaduni sahihi wa Kiislamu na Qur'ani Tukufu.
Mahdi Sotudeh ameashiria nafasi ya vyombo vya habari katika kueneza utamaduni katika jamii ya Kiislamu na akasema: Kueneza utamaduni wa Kiislamu na thamani aali za kidini katika matabaka mbalimbali ya wananchi hususan tabaka la vijana kunaweza kuzidisha hali ya kijiamini katika matabaka hayo. 373077
captcha