IQNA

Mashindano ya awali ya kimataifa ya Qur'ani na hadithi yaanza katika mji wa Qum, Iran

21:05 - March 05, 2009
Habari ID: 1752142
Mashindano ya awali ya kimataifa ya kusoma Qur'ani na hadithi ya olimpiadi ya 14 yanayosimamiwa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Mustafa yalianza jana Jumatano katika mji wa Qum nchini Iran.
Mkuu wa Kamati ya Utamaduni ya mashindano ya 14 ya Qur'ani na hadithi ya chuo cha Mustafa Ismail Piirniya amesema kuwa mashindano hayo yanajumuisha nyanja za kusoma Qur'ani, na kuhifadhi juzuu tofauti za kitabu hicho.
Ismail Piirniya amesema kuwa awamu ya mwisho ya mashindano hayo itafanyika tarehe 7, 8 na 9 za mwezi huu wa Machi yakiwashirikisha makarii kutoka nchi mbalimbali duniani ambao tayari wameanza kuwasili nchini Iran. Wasomaji Qur'ani kutoka nchi za Albania, india, Thailand, Indonesia, Nigeria, Kosovo, Tanzania, Pakistan, Uturuki, Comoro, Azerbaijan na Lebanon wamekwishawasili katika mji mtakatifu wa Qum kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano hayo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa mashindano ya maandishi ya Qur'ani na hadithi yalianza siku tano zilizopita. 372956
captcha