IQNA

Kutolewa fatuwa katika televisheni za Algeria kupigwa marufuku

17:32 - March 07, 2009
Habari ID: 1752905
Kuongezeka kwa televisheni zinazotoa fatuwa za kidini nchini Algeria kumeipelekea serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku utolewaji wa fatuwa hizo.
Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya watu wanaofuatilia maslahi yao binafsi wamekuwa wakitumia vibaya televisheni za satalaiti kwa kutumia watu wasio na elimu ya kidini ya kutosha kutoa fatuwa za kidini. Jambo hilo limelipelekea Baraza la Elimu la Wizara ya Masuala ya kidini ya Algeria kufanya kikao cha siku mbili na kuamua kutoa amri ya kuzuia kutolewa fatuwa za kidini kupitia televisheni za satalaiti. Washiriki wa kikao hicho wamechunguza madhara ya tabia hiyo ya kutolewa fatuwa kupitia televisheni zilizotajwa na kuamua kutafuta njia nyingine ya kutoa fatuwa hizo kwa ushirikiano na serikali ya Algeirs.
Abdallah Ghulamullah, Waziri wa Masuala ya Kidini wa Algeria amewaambia wasimamizi wa misiki na maimamu wa swala ya Ijumaa kwamba wana wadhifa muhimu wa kuzuia fatuwa zinazotolewa na watu wasiofaa. Pia amesema kuwa Uislamu ni dini rasmi ya Algeria na kwamba misikiti ni sehemu ya serikali. Amesema, utolewaji fatuwa na maamuzi kuhusiana na masuala ya Kiislamu ni jukumu la maimamu wa misikiti. 373632
captcha