Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amezungumza mbele ya umati mkubwa wa wananchi wa Sudan akisema kuwa kwa kuchochea utolewaji wa waranti ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) dhidi ya Sudan, Marekani inataka kusimama mbele ya ushujaa na irada ya taifa hilo la Kiafrika.
Dakta Ali Larijani ameshangazwa na hatua ya Marekani ya kutoa waranti hiyo dhidi ya taifa la Sudan na kuwafumbia macho watawala wa Israel ambao wametekeleza jinai kubwa dhidi ya binadamu na watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Katika siku za hivi karibuni, Wananchi wa Sudan wamekuwa wakifanya maandamano makubwa ya kulalamikia waranti iliyotolewa hivi karibuni na mahakama ya ICC dhidi ya kiongozi wao.373940