IQNA

Ihsanoglu: Uislamu umempa mwanamke hadhi na heshima kubwa

16:44 - March 09, 2009
Habari ID: 1753908
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ehsanoglu amesema kuwa dini ya Kiislamu imempa mwanamke heshima na hadhi mkubwa.
Ihsanoglu ameyasema hayo kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mwanamke iliyosadifiana na tarehe 8 Machi.
Ameashiria kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mwanamke inayosema "Mwanamke na Mwanamume Wako Pamoja katika Kukabiliana na Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana" na akasema, Uislamu ulizungumzia suala ukatili dhidi ya wanawake tangu ulipodhidiri kwa mara ya kwanza na kupinga vikali vitendo kama hivyo.
Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa mwanamke ana nafasi kubwa katika kujenga familia, kulea watoto na kuimarisha maadili mema.
Ekmeleddin Ihsanoglu amesema, hii leo mwanamke amekuwa na mchango mkubwa si katika kutunza nyumba na familia pekee bali pia katika nyanja mbalimbali.
Ihsanoglu amezitaka nchi zote wanachama wa OIC kuheshimu ahadi zao za kuondoa dhulma na ukatili dhidi ya wanawake na kuwapa haki zao za kibinadamu. 374614


captcha