IQNA

Makutano wa Familia katika Sira ya Mtume mjini Damascus

17:27 - March 09, 2009
Habari ID: 1753948
Mkutano wa Familia katika Sira ya Mtume (saw) umefanyika nchini Syria katika Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus.
Mkutano huo umefanyika kwa mnasaba wa maulidi ya Mtume Muhammad (saw) ukihudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu wa mji huo.
Mhadhiri wa chuo kikuu Muhammad Kheir al Shiar na mwandishi Hannan Liham wamehutubia mkutano huo.
Muhammad Kheir al Shiar ameashiria maulidi ya kuzaliwa kwa Nabii Muhammad (saw) na Wiki ya Umoja kati ya Waislamu na akasema, dini ya Kiislamu imetilia maanani mno nafasi ya familia na kubuni sheria madhubuti katika medani hiyo.
Amemtaja Mtume wa Uislamu kuwa ni kigezo cha kuigwa na wanadamu wote katika masuala ya malezi na familia na kuongeza kuwa kwa sasa maadui wa dini hiyo wanalenga sekta ya malezi.
Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amesema kuwa miongoni mwa misingi ya malezi katika Uislamu ni kudhihirisha mapenzi kwa mke, kuwa mpole, mwaminifu na kumuheshimu mwanamke na kujipamba kwa ajili yake.
Muhammad Kheir al Shiar amesisitiza pia juu ya udharura wa kulindwa haki zote za manamke. 374812

captcha