Manouchehr Muttaki ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa Ajili ya Ukombozi wa Palestina Ahmad Jibril na kuongeza kuwa hii leo Palestina inamaanisha, uhai, uadilifu na mapambano.
Amesema kuwa jina la Palestina ndilo tamu na linalopendwa zaidi na wananchi wa Iran na Waislamu kati ya majina ya nchi na mataifa yote duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza tena kuwa Palestina ilizaliwa upya baada ya kushinda katika vita vya siku 22 vya Wazayuni huko Gaza.
Kwa upande wake Ahmad Jibril Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa Ajili ya Ukombozi wa Palestina ameashiria mchango mkubwa wa Iran katika kuwasaidia wananchi wa Palestina na akasema Iran ndiye rafiki wa karibu mno kwa taifa hilo. Amesema, anaona aibu kutokana na matamshi ya baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Iran kuhusu kadhia ya Palestina. Amesisitiza kuwa Iran ya Kiislamu imekuwa ikiwaunga mkono na kuwasaidia Wapalestina tangu ilipoasisiwa. 375783