IQNA

Kutekelezwa sheria za Kiislamu nchini Somalia

14:01 - March 12, 2009
Habari ID: 1755184
Serikali ya Somalia siku ya Jumanne ilikubali kutekeleza sheria za Kiislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa sherika la habarila AFP, Farhan Ali Mahmoud, Waziri wa Habari wa Somalia ametangaza habari hizo na kuongeza kuwa, baraza la mawaziri limechunguza kwa kina na makini pendekezo la kutekelezwa sheria hizo nchini Somalia na hatimaye kuafiki suala la kutekeleza sheria hizo nchini.
Kati ya wanachama 36 wa baraza hilo 20 walishiriki katika upigaji kura ya kupitisha sheria hizo. Kwa mujibu wa Katiba ya Somalia, kila sheria inayopitishwa na baraza la mawaziri inapaswa kutekelezwa.
Rais Sheikh Sharif Ahmad, amebainisha kuridhishwa kwake na kupitishwa kwa sheria hizo na kuongeza kuwa zinaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuleta amani na uthabiti nchini humo na hivyo kukomeshwa vita vya ndani ambavyo vimekuwa vikiendelea tokea mwaka 1991. 376471
captcha