IQNA

Wiki ya Qur'ani kuadhimishwa mjini Karachi

13:55 - March 12, 2009
Habari ID: 1755192
Wiki ya Qur'ani Tukufu na kutukuzwa Ahlul Bait (as) ilianza nchini Karachi siku ya Jumatano kwa kuhudhuriwa na wasomaji wawili mashuhuri wa Qur'ani kutoka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maadhimisho ya wiki hii ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Kiislamu yataendelea hadi Jumanne tarehe 17.
Sherehe za kuadhimishwa minasaba hii miwili muhimu ambapo pia maulidi ya Mtume Mtukufu (saw) inaadhimishwa, zitafanyika katika misiki na vituo mbalimbali vya kidini vya mji huo wa Pakistan.
Sherehe hizo zinafanyika kwa ushirikiano wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vilevile Taasisi ya Qur'ani ya Karachi. 376684
captcha