IQNA

Mashindano ya taifa ya Qur'ani yafanyika Ghana

16:38 - March 16, 2009
Habari ID: 1756594
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani yamefanyika mjini Acra nchini Ghana yakisimamiwa na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Acra.
Mashindano hayo yaliwashirikisha wasomaji 30 mashuhuri kutoka mikoa 9 ya Ghana. Mashindano hayo yalihusisha nyanja za kusoma Qur'ani nzima, juzuu 15 na kiraa ya Qur'ani Tukufu.
Kwa mara ya kwanza wasomaji Qur'ani wa kike pia walishiriki katika mashindano hayo na kufanikiwa kushinda nafasi za kwanza.
Mashindano hayo ya taifa ya Qur'ani yamesimamiwa na majaji wa Kighana. 378202

captcha