IQNA

Katibu Mkuu wa OIC atembelea Gaza

15:30 - March 17, 2009
Habari ID: 1756738
Ekmeledin Ihsanoglou, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, ametembela eneo la Ukanda wa Gaza ili kukagua uharibifu uliofanywa na utawala haramu wa Israel katika hujuma yake ya kinyama ya hivi karibuni katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya World Bulletin, katibu Mkuu huyo wa OIC amewasili katika Ukanda wa Ghaza ili kujadiliana na viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, kuhusiana na njia za kukarabati uharibifu uliofanywa na Wazayuni katika hujuma hiyo na pia kutathmini misaada ya kibinadamu kwa watu wanaoihitajia.
Akizungumza na waandishi habari kufuatia safari yake hiyo, Ihsanoglou amebainisha furaha yake kuhusiana na juhudi zinazofanywa na makundi ya Palestina kwa madhumuni ya kurejesha amani na utulivu katika ardhi zao na kutumai kuwa, mazungumzo hayo yatachangia yale yaliyofikiwa huko nyuma kwa lengo la kurudisha amani ya kudumu katika ardhi hizo. Akizungumza katika mkutano huo wa waandishi habari, Muhammad al-Qaul, Waziri wa Sheria wa Hamas amesema kwamba safari hiyo ya Katibu Mkuu wa OIC inathibitisha wazi kwamba Ukanda wa Gaza haujasahaulika na kwamba juhudi za kimataifa zingali zinafanywa kwa madhumuni ya kuondolewa mzingiro wa kidhulma unaotekelezwa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, wa ukanda huo.
Katika mashambulio yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, raia wapatao 1500 walipoteza maisha yao na wengine zaidi ya 5300 kujeruhiwa. 378412
captcha