IQNA

Jihadi, amana ya mashahidi wa Palestina

15:36 - March 17, 2009
Habari ID: 1756741
'Hivi Karibuni tumeshuhudia ushindi wa watu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya Wazayuni na harakati ya Hamas imeweza kuthibitisha wazi ushindi wa Uislamu dhidi ya batili. Kwa msingi huo, mashahidi ambao walitutangulia wametuachia amana yenye thamani kubwa ambayo si nyingine bali ni jihadi.'
Hayo yamesema na Swalah az-Zawawi, Balozi wa Palestina nchini Iran.
Akizungumza katika kikao cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu mjini Tehran, Az-Zawawi amesema kuwa lengo la Waislamu wote ni moja. Amesema, Wazayuni ni adui wa pamoja wa Waislamu wote na kuongeza kwamba, Wazayuni ambao wanaungwa mkono kwa kila njia na nchi za Magharibi, wana lengo la kupora ardhi zote za Wapalestina, lakini kwamba Wapalestina hawatawaruhusu kufikia lengo hilo kirahisi.
Az-Zawawi amesisistiza kwamba nchi za Magharibi zinataka kuidhihirisha Iran, ambayo inatetea kwa dhati maslahi ya umma mzima wa Kiislamu kuwa ni adui wa nchi za Kiarabu, lakini kwamba Waislamu walio na muamko kamwe hawatahadaika na njama hiyo.
Balozi wa Palestina mjini Tehran amezitaka nchi za Kiislamu kufanya kila ziwezalo ili kuwasadia Wapalestina kufikia lengo lao la mwisho la kurejesha haki zao kutoka kwenye makucha ya Wazayuni na kuunda taifa lao huru, mji mkuu wao ukiwa ni Baitul Muqaddas, na pia kuwafikisha watenda jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC huko the Hague. 378467
captcha