Amesema, msomaji huyo wa Misri amekuwa nyota katika fani ya usomaji Qur'ani kwa kipindi cha miaka 100 iliyopita.
Hayo yamesemwa na Sayyid Mahdi Fatimiyan, aliyehifadhi Qur'ani nzima na ambaye pia ni refa wa usomaji Qur'ani katika mazungumzo yake na shirika la IQNA. Amesema Qur'ani ni muujiza ambao una pande mbalimbali ukiwemo upande na sifa ya usomaji wake kwa sauti ya kuvutia na kwamba hadi siku ya Kiama hakuna kitabu kingine kinachoweza kushindana na kitabu hicho kitakatifu wala kudai kwamba kina uwezo wa kumuongoza mwanadamu kwa njia inayofaa. Sayyid Mahdi Fatimiyan ameendelea kusema kuwa, lahani na sauti ni moja ya sifa za kuvutia za Qur'ani na kwamba katika kipindi chote cha historia wasomaji wa kitabu hicho wameweza kuwavutia watu kimaanawi kutokana na sauti tofauti na za kuvutia za usomaji wake, jambo ambalo limewafanya wengi kusilimu. 374256