Kwa mujibu wa hati hiyo ya maelewano ambayo pia imetiwa saini na Kamati ya Taifa ya Waislamu wa Nepal, serikali ya nchi hiyo imeahidi kubadili vipengee vya Katiba na kutunga sheria zitakazoilazimisha kutambua rasmi haki za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni za Waislamu.
Pande hizo mbili pia zimekubaliana kuunda kamati maalumu ya kuboresha hali ya jamii ya Kiislamu, kuanzisha kamati ya hija na baraza la shule za Kiislamu nchini Nepal.
Serikali ya Nepal vilevile imeahidi kuchunguza uwezekano wa kutangazwa likizo ya taifa katika sikukuu za Kiislamu.
Wakati huo huo Kamati ya Taifa la Waislamu wa Nepal imefuta maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa na Waislamu wa nchi hiyo dhisi ya serikali na kutangaza kuwa itashirikiana na serikali katika kutunga Katiba mpya.
Nepal ambayo ni nchi ndogo iliyoko kati ya nchi mbili kubwa za India na China ina jamii ya watu milioni 23 wengi wao wakiwa ni wafuasi wa dini za Kihindu na Kibuddha. Waislamu wanaunda asilimia 4 tuu ya jamii ya Nepal. 379070