Nabih Berri ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa kuwaenzi wanazoni wawili wa Kiislamu Abdullah al Alaayili na Sheikh Muhammad Jawad Mughniya unaofanyika mjini Beirut. Amesema kuwa miongoni mwa matunda ya fikra za wanazuoni hao wawili wa Kiislamu ni kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii za Kiislamu.
Spika wa Bunge la Lebanon amesema kuwa wanazuoni hao wawili wanamageuzi waliasisi mfumo wa uchunguzi wa masuala ya kihistoria na kifiqhi na kuimarisha umoja na mshikamano kati ya madhehebu za Kiislamu.
Amesisitiza kuwa dunia ya leo imechoshwa na ulimwengu wa kambi moja na kuongeza kuwa serikali za kibeberu zimekuwa zikifeli katika mitihani yote kuanzia Gaza hadi Iraq. 380203