IQNA

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah:

Iran ni nchi muhimu katika mapambano dhidi ya Uzayuni

17:08 - March 26, 2009
Habari ID: 1758116
Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naeem Qasim amesema kuwa ushirikiano wa nchi za Kiarabu na Kiislamu utainufaisha Lebanon na kusisitiza kuwa Iran ni nchi muhimu katika mapambano dhidi ya ubeberu na Uzayuni.
Sheikh Naeem Qasim ameyasema hayo mjini Beirut katika mkutano wa kuwaenzi wanazuoni wawili wa Kiislamu Sheikh Abdullah al Alaaili na Ustadh Muhammad Jawad Mughniya. Amesisitiza kuwa mapambano ndio njia pekee na kukabiliana na njama za maadui.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeshindwa kuchora mipaka yake na kutambuliwa rasmi katika eneo la Mashariki ya Kati licha ya njama zote za kimataifa.
Amesema kuwa suala la Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni suala la Kiislamu na kibinadamu na kuongeza kuwa, ulimwengu wa Kiislamu umekuwa na umoja na mshikamano na kwamba ushahidi wa ukweli huo ni mapambano ya Waislamu wa Kishia nchini Lebanon na mapambano ya Kisuni ya Waislamu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya wavamizi wa Kizayuni.
Amesema kuwa madola ya kibeberu yamefeli katika kuzizingira nchi za Iran, Iraq, Syria, Afghanistan na Lebanon. 380204

captcha