Hayo yamesemwa na Mahdi Adeli, msomaji wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu raia wa Iran na kuongeza kuwa, moja ya sababu ambazo zimepelekea msomaji huyo kuenziwa duniani na hivyo kupata umashuhuri mkubwa katika taaluma ya usomaji Qur'ani, ni utumiaji wake wa lahani mbalibali za kuvutia wakati anaposoma kitabu hicho kitakatifu.
Huku akiashiria vipawa na umahiri mkubwa wa Ismail Mustafa katika taaluma ya usomaji Qur'ani Takatifu, Adeli amesema kuwa umahiri wa msomaji huyo mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu ulimuwezesha kusoma kwa sauti na lahani tofauti za kuvutia kuambatana na maana ya aya alizokuwa akisoma.
Amesema, Mustafa Ismail amekuwa mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na juhudi zake kubwa alizofanya kwa madhumuni ya kuboresha sauti na lahani zake katika usomaji wa Qur'ani, na hasa kuhusiana na sura za Najm, Qamar, Rahman, Qaf, Hujuraat na Maryam. 374620