Kikao hicho kimehudhuriwa na shakhsia na wanafikra mbalimbali wa Kiislamu na Kikristo kutoka nchi za Asia na Ulaya.
Licha ya kuchunguza na kujadili sifa muhimu na za kuvutia za Imam Ali (as), wazungumzaji wa kikao hicho wameashiria aya mbalimbali za Qur'ani Tukufu na kuwataka Waislamu kote duniani kuzingatia umoja na mshikamano miongoni mwao kwa ajili ya kukabiliana na njama za maadui wa dini hiyo.
Wamezungumzia utukufu na elimu kubwa aliyokuwa nayo kiongozi huyo wa Uislamu na kusema kuwa, licha ya elimu hiyo yote lakini ni watu wachache mno waliopata kunufaika na elimu hiyo pamoja na kutambua nafasi yake rasmi na halisi katika jamii kutokana na baadhi ya masuala yaliyotawala katika zama za uhai wake. 380246