IQNA

Kufunguliwa Kituo cha Qur'an nchini Singapore

11:54 - March 28, 2009
Habari ID: 1758322
Kwa kumalizika shughuli za ukarabati wa msikiti wa zamani wa Siglip katika mji wa Singapore nchini Singapore, Kituo cha Darul Qur'an ambacho kilifunguliwa siku ya Ijumaa, kitatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Kiislamu na yanayuhusiana na Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa gazeti la Straits Times, kituo hicho ambacho kina maktaba, sehemu ya kuendeshea masomo na michezo, kitatumika pia kwa ajli ya kuwafunza wataalamu wa Qur'ani. Kufikia sasa wanafunzi wapatao 1000 wamesajili majina yao kwa lengo la kupata masomo katika kituo hicho.
Katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho, Allama Musa, Mkuu wa Baraza la Waislamu la Singapore ameashiria umuhimu wa kuzingatia na kutadabari aya za Qur'ani na kuongeza kuwa, licha ya kuwa misikiti yote ya Singapore inatoa masomo ya msingi kuhusiana na Uislamu lakini kituo hicho kipya cha Qur'ani kitajihusisha na masuala ya kulea na kuwafunza wataalamu waliobobea katika masuala ya kitabu hicho kitakatifu. Amesema, katika ulimwengu wa leo, kuna udharura wa kuelewa vyema na kwa kina aya za Qur'ani ili kuzuia kutolewa tafsiri potofu na zisizo sahihi kuhusiana na aya za kitabu hicho.
Singapore ni nchi ndogo sana iliyo kati ya Malaysia na Indonesia, kusini mashariki mwa Asia, ambayo asilimia 15 ya wakazi wake ni Waislamu. 380557
captcha