IQNA

15:14 - April 04, 2009
Habari ID: 1760077

Filamu ya Misikiti ya Paris kuonyeshwa mjini Marseille

Filamu ya matukio ya kweli (Documentary) kuhusu misikiti ya Paris inatarajiwa kuonyeshwa mjini Marseille tarehe kumi Aprili.

Filamu hiyo inamulika zaidi juu ya nafasi ya misikiti katika maisha ya mtu binafsi na jamii ya Waislamu wa Ufaransa. Watengenezaji wa filamu hiyo wametumia mitazamo ya viongozi wa Kiislamu kuhusu maeneo hayo matakatifu.
Filamu ya “Misikiti ya Paris” imetengenezwa na Jean-Michel Riera chini ya usimamizi wa msikiti mkuu wa Paris. 382463
captcha