Kikao hicho ambacho kilisimamiwa na OIC mwishowe kiliamua kuasisi ofisi maalumu itakayosimamia shughuli za misaada ya kibinadamu itakayoendesha shughuli zake chini ya umoja huo.
Akizungumza katika kikao hicho Muhammad Ahmad as-Sharif, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Tablighi ya Kiislamu amesema kuwa kuna baadhi ya mashirika ya misaada ya kibinadamu yasiyo ya Kiislamu ambayo yanaendesha shughuli zao katika nchi za Kiislamu na kwamba kikao hicho cha pili kimefanyika kwa ajili ya kuainisha msimamo wa OIC kuhusiana na suala hilo na kutafuta njia za kusimamisha madhara ya mashirika hayo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC amesema katika kikao hicho kwamba, masuala yaliyojadiliwa yanafungua upeo mpya wa ushirikiano kati ya mashirika rasmi na yasiyo rasmi ya OIC.
Katika kikao hicho cha Libya wawakilishi 50 wa mashirika ya misaada ya kibinadamu ya zaidi ya wanachama wa OIC walishiriki na kutoa maoni yao tofauti kuhusiana na jinsi ya kuimarisha shughuli zao mwa manufaa ya umma wa Kiislamu. 382394