IQNA

Kuwait yaandaa mashindano ya Qur'ani nchini Ubelgiji

17:54 - April 04, 2009
Habari ID: 1760172
Ubalozi wa Kuwait mjini Brussels Ubelgiji umepanga kuandaa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani nchini humo tarehe 18 Aprili, kwa jina la Swabah Ahmad al-Jabir as-Swabah.
Nabila al-Mala, Balozi wa Kuwait nchini Ubelgiji amesema kwamba mashindano hayo yatafanyika kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiislamu na Utamaduni cha Msikiti wa Brussels, ambapo jamii za Waislamu waliowachache wanaoishi nchini humo wanatazamiwa kushiriki. Amesema mashindana hayo yameandaliwa kwa ajili ya kuanzisha mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa jamii hizo za Kiislamu. Ubalozi huo umekuwa ukiandaa na kutekeleza ratiba mbalimbali katika minasaba mbalimbali ya kidini.
Matokeo ya mashindano hayo yatatangazwa wiki moja baada ya kufanyika ambapo washindi watatunukiwa zawadi nono. 382426
captcha