IQNA

Mkutano wa kimataifa wa Tunu ya Ulimwengu wa Kiislamu katika Masuala ya Wanawake

11:23 - April 05, 2009
Habari ID: 1760379
Muhula wa kutuma makala katika mkutano wa kimataifa wa "Tunu ya Ulimwengu wa Kiislamu katika Masuala ya Wanawake, Uchunguzi wa Athari za Feminism" unamalizika tarehe 19 mwezi huu wa Aprili.
Mkutano huo unafanyika kwa mara ya pili sasa ukisimamiwa na kitengo cha wanawake katika ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei.
Lengo la mkutano huo ni kuwaeleza walimwengu nafasi halisi ya wanawake katika Uislamu, kuchambua na kukosoa nafasi ya wanawake katika dunia ya sasa.
Masuala yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa kimataifa ni pamoja na fikra za Kiislamu kuhusu haki za mwanamke, nafasi ya taasisi ya familia, athari mbaya za fikra za mfumo wa feminism na kadhalika. 382402
captcha