Mashindano ya kila mwaka ya Qur'ani kufanyika Syria
Mashindano ya kila mwaka ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kufanyika katika wiki ya mwisho ya mwezi Julai mwaka huu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Washiriki katika mashindano hayo watachuana katika kuhifadhi juzuu 5, juzuu 10 na Qur'ani kamili.
Washiriki katika mashindano ya kusoma Qur'ani wanalazimika kuwa na ujuzi wa sheria za tajwidi na sauti ya kuvutia.
Mashindano hayo yanafadhiliwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus. 383033