IQNA

Iran yalaani mauaji ya Mashia nchini Pakistan

14:24 - April 07, 2009
Habari ID: 1761416
Huku akisisitiza kwamba misikiti ni sehemu ya ibada na sio ya mauaji, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mauaji yaliyotekelezwa hivi karibuni na magaidi wa Pakistan dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa nchi hiyo.
Akizungumza mbele ya waandishi habari, Hassan Qashqavi, amesema kuwa misikiti ni sehemu takatifu ya ibada kwa Waislamu wote bila kujali usunni wala ushia wao.
Akijibu swali kuhusiana na madai ya gazeti moja la Uingereza kuhusiana na uwezekano wa utawala haramu wa Israel kuishambulia Iran, Qashqawi amesema kuwa madai kama hayo ni propaganda na vita vya kisaikolojia tu vya Wazayuni dhidi ya Iran, vita abavyo si rahisi kutekelezwa kivitendo. Qashqawi amekumbusha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitangaza mara kwa mara kwamba iko tayari kutetea na kulinda ardhi na maslahi yake dhidi ya hujuma ya aina yoyote ile ya maadui.
Kuhusiana na matamshi ya hivi karibuni ya Rais Barack Obama wa Marekani kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran unaotekelezwa kwa malengo ya amani, Qashqavi amesema kuwa maneno ya viongozi wa Marekani kwamba wanaheshimu haki ya Iran ya kunufaika kwa amani na teknolojia hiyo ya kisasa hayatoshi na kwamba yanapaswa kutekelezwa kivitendo. Amesisitiza kwamba silaha za nyuklia haziko kwenye mfumo wa ulinzi wa Iran na kwamba nishati ya nyuklia inafuatiliwa na taifa la Iran kwa malengo ya amani. 383643
captcha