Amnesty International imetoa ripoti iliyoiwasilisha kwa Umoja wa Mataifa ikieleza ukandamizaji na uvunjaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Saudi Arabia kama vile kutiwa mbaroni na kushikiliwa kiholela, kukatiwa hukumu zisizo za kiadilifu na mateso mengine katika kipindi cha miaka iliyopita.
Amnesty International imewasilisha ripoti yake hiyo kwa Umoja wa Mataifa kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia kabla ya kuanza mkutano wa umoja huo uliopangwa kufanyika hii leo Jumatatu huko Geneva, Uswisi kuchunguza hali ya haki za binadamu huko Saudia. Shirika hilo la kutetea haki za bninadamu limetaka kuchukuliwa hatua serikali ya Riyadh kutokana na kutotekeleza majukumu yake kuhusu haki za binadamu.
Ukandamizaji mwingine uliotajwa kwenye ripoti hiyo ni kuhusu wimbi jipya la ukandamizaji dhidi ya wananchi huko Saudi Arabia katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni. 1306046