IQNA

Mashindano ya Qurani Tukufu kufanyika Bahrain

17:09 - April 08, 2009
Habari ID: 1762202
Mashindano ya taifa ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu yaliyopewa jina la “al Dhikrul Hakim” yanatarajiwa kuanza tarehe 17 Aprili nchini Bahrain.
Mashindano hayo yanasimamiwa wanaharakati wa masuala ya Qur’ani, kwa kushirikiana na gazeti la al Wasat, kituo cha kibiashara cha Abdunnabi na Chuo cha Qur’ani cha Bahrain.
Washiriki katika mashindano hayo watachuana katika kusoma, kuhifadhi, kufasiri aya za Qur’ani, visa vifupi na sanaa ya Qur’ani Tukufu.
Awamu ya awali ya mashindano hayo inawashirikisha watu 110 na washindi watafanikiwa kuingia fainali ya kitaifa kusoma na kuhifadhi Qur’ani.
384266
captcha