IQNA

Obama: Marekani si adui wa ulimwengu wa Kiislamu

17:08 - April 08, 2009
Habari ID: 1762204
Rais Barack Obama wa Marekani amehutubia Bunge la Uturuki na kufanya jitihada za kuboresha uhusiano wa nchi yake na nchi za Kiislamu.
Obama amesisitiza kwamba Marekani si adui wa ulimwengu wa Kiislamu.
Obama ameeleza uungaji mkono wake kwa suala la kuanzishwa dola huru la Palestina na kujaribu kupunguza ufa uliopo kati ya nchi za Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu.
Amesema kuwa atafanya jitihada za kukuza ushirikiano na nchi za Kiislamu kwa kuzingatia maslahi ya pande mbili na misingi ya kuheshimiana.
Rais Barack Obama amesema kuwa moja ya malengo ya serikali yake ni kurejesha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati. 384242
captcha