IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Amir Sulaiman kufanyika Saudi Arabia

11:55 - April 12, 2009
Habari ID: 1763535
Mashindano ya 11 ya taifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Amir Sulaiman yamepangwa kufanyika baadaye mwezi huu nchini Saudi Arabia.
Salman al Amri ambaye ni miongoni mwa wasimamizi wa mashindano hayo amesema kuwa awamu ya kwanza ya mashindano ya Amir Sulaiman itafanyika katika maeneo mbalimbali ya Saudi Arabia na washindi watano wa kwanza watafaulu kuingia fainali.
Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani yanasimamiwa na Idara ya masuala ya Kiislamu ya Saudia.
Watayarishaji wa mashindano hayo wamewahidi kutoa zawadi nono kwa washindi wa mashindano hayo.
Watu wote wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo wanalazimika kuwa wamejiandikisha kufikia tarehe 18 Aprili. 386015

captcha