IQNA

Wamagharibi wanatoa picha isiyokuwa sahihi kuhusiana na Iran

14:35 - April 12, 2009
Habari ID: 1763538
Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vimekuwa vikitoa mtazamo na picha isiyokuwa sahihi kuhusu Iran na taifa la nchi hiyo kwa kutumia visingizio mbalimbali kama shughuli za nyuklia za Iran.
Hayo yamesemwa na mtengeneza filamu maarufu wa Iran Majid Majidi ambaye ameongeza kuwa Wamagharibi wanapaswa kuonyeshwa picha tofauti na ile inayoonyeshwa kwenye vyombo vya habari vya nchi zao kuhusu Iran. Amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya habari vinapuuza historia na utamaduni tajiri wa Iran wakati vinapozungumzia nchi hiyo.
Majid Majidi amesema kuwa si kazi sahihi kutazama kila kitu kwa kutumia jicho la masuala ya kisiasa na kwamba mwenendo huo ndio sababu ya kuonyeshwa picha isiyokuwa sahihi kuhusiana na Iran na watu wake katika vyombo vya habari. 386215

captcha