Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamisha Swala ya Chuo Kikuu Huria cha Kiislamu cha Azadi Aliridha Salihi amesema kuwa mkutano huo utafanyika kwa lengo la kujadili na kubadilisha tajiriba kati ya wanachuo wa Kiislamu katika medani ya Qur'ani na swala. Ameongeza kuwa kwa sababu hiyo Chuo Kikuu Huria cha Kiislamu cha Azadi ambacho ni Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la vyuo vikuu vya ulimwengu wa Kiislamu, kimeazimia kuitisha mkutano huo wa kimataifa wa Swala na Qur'ani kama hatua yenye taathira kubwa katika uwanja huo.
Amesema maandalizi ya mkutano huo yamekwishaanza.
Salihi amesema kuwa mkutano huo utajadili maudhui za Qur'ani, swala na Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw). 386767