Kwa mujibu wa tovuti ya Artdaily athari au kazi zitakazowasilishwa katika maonyesho hayo zitasisitiza juu ya irfani ya Kiislamu kwa kujadili masuala kama vile nuru katika irfani ya Kiislamu, sifa za usufi, mashairi ya kiirfani na athari za irfani ya zamani na ya zama hizi. Mashairi ya Maulana yaliyotarjumiwa kwa lugha ya Kiingereza ni miongoni mwa mambo yatakayoonyeshwa katika maonyesho hayo. 387495