Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la ar-Rai, Yusuf as-Swamini mmoja wa viongozi wanaoandaa mashindano hayo amesema kuwa usajili wa majina ya washiriki wa mashindano hayo umeanza siku mbili zilizipota na kwamba watu walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kufahamu jinsi usajili huo unavyoendeshwa kupitia kamati inayoshughulikia mashindano hayo.
As-Swamini amesema kuwa masharti ya kushiriki katika mashindano hayo ni washiriki kuwa raia wa Kuwait waliohifadhi vyema Qur'ani. Pia amesema kuwa washiriki hawapasi kuwa ni maimamu wa miskiti na waadhini wa Wizara ya Wakfu ya Kuwait wala washindi wa mashindano ya Qur'ani ya miaka iliyopita ili kutoa fursa kwa makundi mengine ya washindani. Amesema kuwa washindi watapewa zawadi nono katika sherehe maalumu za kuhitimisha mashindano hayo. 387396