Mashindano hayo yaliwashirikisha watu 90 kutoka maeneo mbalimbali ya Imarati wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 21.
Hamad Muhammad Abdulrahman ambaye ni miongoni mwa wasimamizi wa mashindano hayo amesema kuwa washindani walichuana katika kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 20, juzuu 10 na juzuu 5. Ameongeza kuwa kamati ya majaji wa mashindano hayo inachunguza utendaji wa washiriki na itaainisha washindi hapo baadaye.
Mashindano ya taifa ya kuhifadhi Qur'ani ya Vituo vya Maktum yalianza Ijumaa tarehe 10 Aprili yakisimamiwa na Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai. 388078