IQNA

Majlisi ya kisomo cha Qur'ani kufanyika katika haram ya Abdul Adhim al Hassani (as)

12:02 - April 15, 2009
Habari ID: 1765256
Majlisi ya kisomo cha Qur'ani Tukufu ya wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Iran imepangwa kufanyika katika haram ya Abdul Adhim al Hassani katika viunga vya jiji la Tehran.
Majlisi hiyo itahudhuriwa na wasomaji Qur'ani wa kimataifa wa Iran kama Mahdi Farshikhlou na Qasim Radhi na wahifadhi wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Majlisi hiyo ya kisomo cha Qur'ani itafanyika Ijumaa ya wiki hii katika msikiti mkuu wa mji wa Rei katika haram ya Abdul Adhim al Hassani.
Pembeni mwa majlisi hiyo ya kisomo cha Qur'ani kutafanyika mashindano ya elimu na maarifa ya Qur'ani Tukufu.
Majlisi hizo zimekuwa zikifanyika kila siku ya Ijumaa katika msikiti mkuu wa Rei baada ya swala ya magharibi. 388206

captcha